Rais
amezungumza hayo wakati wa maombi maalum ya kuomboleza kifo cha msaidizi wa
Mkuu wa Jeshi la Polisi Uganda, Felix Kaweesi huko Kulambiro, nje ya mji wa
Kampala na kueleza lengo lake kubwa hivi sasa ni kuwasaka na kuwaua wale
anaodai ni wahalifu.
Hivi
karibuni watu wasiojulikana waliwapiga risasi na kuwaua maafisa wa jeshi
akiwemo kamanda Kaweesi ambae pia alikuwa msemaji wa jeshi hilo.
Taarifa za
jeshi la polisi zilisema kuwa mlinzi na dereva wake waliuawa pia katika
shambulio hilo,
Kadhalika
Rais ametoa agizo kwa maafisa wake wenye silaha bila ya kusita kumpiga risasi
mtu yoyote wanaemshuiku kwamba ana silaha na anania ya kuwashambulia.
Museveni pia
amedai kuwa baadhi ya polisi ni majambazi na kuwataka polisi kujichunguza kwani
ana imani wako ambao wanaua raia.
Amewataka
raia walio na taarifa muhimu kuripoti akiwashutumu maafisa wa usalama kuwa
hawaaminiki.
Akionekana
mwenye hasira, Museveni amesema wale wanaoua watu nchini Uganda kwa kutumia
bunduki wakitumia usafiri wa pikipiki ni nguruwe na amesisitiza nguruwe hao
watauawa.
Museveni pia
ametishia kupunguza idadi ya wahudumu wa boda boda jijini Kampala, akisema
wahudumu hao Sasa wanatumika na wahalifu.
Museveni pia
amechukua fursa hiyo kuonya watumishi wa umma dhidi ya kudai nyongeza ya
mishahara akisema wanaofanya hivyo wanajitafutia matatizo.
Kwake
Museveni, mishahara kwa wafanyakazi ndio inayolemaza juhudi zake za kuekeza
katika usalama kwani kiasi kikubwa cha Pesa kinatumika kulipa mishahara.
Ameamrisha
mamlaka jijini kampala katika Nchi na miji ilioendelea kama New York.
Kwake
Museveni, mbinu zinazotumika kukabiliana Na wahalifu nchini Uganda ni za
zamani, ikiwa pamoja na kuwauliza walioshuhudia kuweka kamera za CCTV katika
jiji lote ili kuwanasa wahalifu kwa haraka, akisema hiyo ndiyo mbinu ya kisasa
inayotumika.
No comments:
Post a Comment