China na
Umoja wa ulaya ambao ni wateja wakubwa wa nyama toka Brazil,wamesimamisha
uagizaji wa nyama kwa tuhuma kwamba makampuni yamekuwa yakiwauzia nyama ambazo
sio salama kwa miaka mingi.
Nchi ya
China imepiga marufuku kabisa uingizaji wa nyama nyekundu kutoka Brazil, wakati
Umoja wa Ulaya ikitangaza kuacha kununua nyama, kuku na bidhaa nyingine kutoka
makampuni yaliyohusika na kashfa.
Siku ya
Ijumaa, polisi wa nchini Brazil walivamia ofisi kubwa za makampuni
yanayozalishwa nyama na nchi humo
Makampuni
hayo yametuhumiwa kuuza nyama iliyooza na kuwahonga waandamizi viongozi wa
serikali.
No comments:
Post a Comment