Kiongozi wa
kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa
"dhambi na makosa yaliyotekelezwa na Kanisa na waumini wake … ambao
walitekwa na chuki na ghasia" wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda.
Alikuwa
akiongea baada ya kukutana na Rais Paul Kagame mjini Vatican.
Ombi lake la
msahama limetokea baada ya ombi la Rwanda Novemba mwaka jana kwa Vatican kuomba
radhi kutokana na mchango wa mapadri wa kanisa Katoliki na baadhi ya viongozi
wake wakati wa mauaji hayo ya mwaka 1994.
Kwa mujibu
wa Vatican Radio, Papa pia "ameelezea nia yake kwamba kutambua udhaifu huu
wa kanisa kipindi hicho, ambao, uliathiri sana sifa za Kanisa, kunaweza
kuchangia 'kutakaswa kwa kumbukumbu' na kuendeleza, kwa matumaini na uaminifu,
amani siku za usoni."
Wakati wa
mauaji hayo yaliyodumu siku 100, Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa
kadiri waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo
yalitekelezwa hadi katika makanisa ambapo watu walikuwa wamekimbilia kutafuta
hifadhi.
No comments:
Post a Comment