Mkurugenzi
wa shirika la ujasusi la Marekani FBI James Comey, amethibitisha kwa mara ya
kwanza kabisa kuwa FBI inaendesha uchunguzi wa madai kuwa Urusi iliingilia kati
uchaguzi wa mwaka 2016.
Hii inahusu
uchunguzi wa kuwepo uwezekano wa uhusiano kati ya watu kwenye kampeni ya Trump
na serikali ya Urusi, na ikiwa kulikuwa ushirkiano kati ya kampeni ya Trump na
Urusi.
FBI pia
itachunguza ikiwa uhalifu ulifanyika. Trump hata hivyo amekana kuhusika kwa
njia yoyote.
Urusi mara
nyingi imekana majaribio ya kushawishi uchaguzi wa Marekani.
Wakuu wa
ujasusi Marekani kutoa ushahidi
Barua pepe:
Jaji amtaka Clinton kujibu mashtaka
Uchaguzi
Marekani: Nani atashinda?
Mkurugenzi
huyo wa FBI alikuwa akizungumza katika kikao kisicho cha kawaida cha kamati ya
bunge la Congress, ambayo pia inachunguza uwezekano wa kuwepo ushirikiano kati
ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.
Bwana Comey
alisema kuwa uchunguzi huo ni mgumu na kuongeza kuwa hawezi kuipa kamati hiyo
taarifa za kina ambazo bado hazijatolewa kwa umma.
Pia alisema
kuwa hawezi kutoa tarehe ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
Pia
aliyefika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa sharika la kitaifa linalohusika na
ulinzi NSA Mike Rogers.
Alisema kuwa
NSA inaunga mkono ripoti iliyochapisjwa mwezi Januari, ambayo ilisema kuwa rais
wa Urusi Vladimir Putin, alikuwa ameamrisha harakati za kuvuruga kampeni za
mshindani wa Trump, Hillary Clinton.
Maafisa wote
hao pia walikana madai yaliyoandikwa kwenye mtandoa wa Twitter mapema mwezi huu
na bwana Terump, kuwa rais wa zamani Barack Obama aliamrisha kufuatiliwa kwa
mawasiliano kwenye jumba la Trump Tower.
Mwezi
Januari mashirika ya ujasusi nchini Marekani yalisema kuwa Urusi iliwasaidia
wadukuzi wa mitandao kudukua akaunti za barua pepe za maafisa wa juu wa
Democrat ambao walifichua taarifa za aibu kumsaidia Trump kumshinda Hillary
Clinton.
No comments:
Post a Comment