Waziri wa
ulinzi wa Poland, Antoni Macierewicz amemshutumu Donald Tusk kwa kusaliti
maslahi ya nchi, kuhusu ajali ya ndege ya Smolensk iliyotokea mwaka 2010 na
kugharimu maisha ya aliyekuwa Rais wa Poland Lench Kaczynski na watu wengine
95.
Bwana Tusk,
ambaye sasa ni rais wa Umoja wa Ulaya, alikuwa waziri mkuu wakati
huo.Macierewicz amekosoa uamuzi wa Tusk kuchagua Urusi kuongoza uchunguzi
kuhusu tukio hilo.
Adhabu
inayotokana na uhaini wa kidiplomasia ni kifungo cha miaka 10 gerezani.
Ofisi ya
mwendesha mashtaka nchini Poland ana siku thelathini kuamua kama ufanyike
uchunguzi kuhusu shutuma hizo.
Hizi ni
jitihada mpya za chama cha Law and Justice katika kuharibu sura ya Tusk.Mapema
mwezi huu Chama hicho kilipinga vikali kitendo cha Tusk kuchaguliwa tena
kuongoza umoja wa ulaya kwa awamu ya pili.
No comments:
Post a Comment