Msemaji wa
polisi amehakikisha kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uchunguzi unaendelea,
wakati ambapo moja ya mashirika makuu yanayotetea haki za binadamu nchini Burundi,
Ligue Iteka, lililopigwa marufuku tangu mwanzoni mwa mwaka huu, limebaini
kwamba machafuko na visa vya mauaji vimeongezeka nchini humo, huku likisema
ukandamizaji huo unaendeshwa na vikosi vya usalama vinavyounga mkono utawala wa
Pierre Nkurunziza, vikosi ambavyo vinaoongozwa kwa idadi kubwa na kundi la
zamani la waasi la CNDD-FDD.
Miili ya
watu waliouawa kikatili imeendelea kugunduliwa sehemu mbalimbali nchini
Burundi.
Kwa mujibu
wa shirika la Ligue Iteka, miili 22 ya watu waliouawa iligunduliwa katika mitaa
au misitu kuanzia Januari, 17 hadi Februari 24 na tayari miili 24 imegunduliwa
ndani ya kipindi cha wiki tatu za mwezi huu wa Machi.
Shirika hili
kongwe la haki za binadamu nchini Burundi, limeinyooshea kidole cha lawama
serikali ya Burundi inayoongozwa na chama kutoka kundi la zamani la waasi wa
Kihutu la CNDD-FDD kuhusika na mauaji hayo.
"Mara
nyingi, miili hii ya watu waliouawa haitambuliwi.Hali hii inatutia wasiwasi
mkubwa, na ndio maana kila wiki tunailalamikia kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia
kati. "
Makamu wa
kwanza wa rais nchi Burundi, Gaston Sindimwo amekosa tuhuma hizo, huku
akihakikisha kwamba "usalama umeimarika,".
Kuhusu ombi
la uchunguzi huru, gaston Sindimwo hataki kusikia hilo, akibaini kwamba Burundi
ina wachunguzi wazuri
No comments:
Post a Comment