
Upande wa Jamuhuri umeiomba
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya
Afisa usalama wa Taifa na kujipatia chakula katika hotel moja ya
kimataifa jijini Arusha inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo
Bw.
Akitoa ombi hilo Wakili wa Serikali
Bi. Grace Madikenya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, Mhe.
Gwantwa Mwakuga, alisema upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo
sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18.
“Sasa tumeona tutamtesa mteja
wetu. Hivyo kwa nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana
miezi hii 18 ni mwaka mmoja na miezi sita,”alisema.
Ombi hilo lilipingwa vikali
na Wakili wa utetezi, Bi. Edna Haraka na kuiomba mahakama hiyo iendelee na kesi
hiyo, kwa madai kuwa upande wa mwendesha mashitaka unatumia Mahakama kama
kichaka cha kumnyima haki mteja wao na kumnyanyasa.
Alisema upande huo hauna nia njema
na mshitakiwa na kwamba kitendo cha kuiondoa kesi hiyo mahakamani sio mara ya
kwanza ni mara ya pili, ambapo ya kwanza waliomba hivyo na mahakama ilipofuta
walimkamata mteja wao na kumnyima dhamana.
“Sasa leo tupo katika kusikiliza
shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta maelezo ya shahidi na leo
wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee kumyanyasa mteja wetu. Hapana!
Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya kwa kivuli cha
Mahakama,”alisema Edna
Wakili huyo alisema serikali ya
sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri kusikiliza wa BRN, sasa wakati
inafanyika hivyo wengine wanachelewesha kwa sababu zao.
Hakimu Gwantwa Mwakuga baada ya
kusikiliza pande zote mbili, alisema atatoa uamuzi Aprili 28 mwaka huu,
ya kama anakubali shauri liondolewe au la.
Bw. Lengai anakabiliwa na
shitaka la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na
malazi kwenye Hotel ya kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment