
Na
Daudi Manongi-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa
madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2015/2016 na 2016/17.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini
Dodoma.
“Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na
fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza
Mhe.Manyanya.
Amesema kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi
Juni, 2016 jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814,
na pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017
jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.
Aidha katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa
kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu
Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema
kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha
madaraja kama inavyotakiwa.
Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika
mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni
wa chuo cha ualimu korogwe.
Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na
mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
No comments:
Post a Comment