
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na
kuuenzi
Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande
Mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo
kama hatua ya kudumisha Muungano huo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Mahojiano na vyombo
Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya
Kwanza zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa
tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa makubwa kwa pande zote Mbili
kwani jamii zimefahamiani na kushirikiano vizuri katika shughuli za kiuchumi na
za kimaendeleo hasa uimarishaji wa ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande
Mbili.
Aidha,Amesema hatua zinazochukuliwa
za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani
linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa unakuwa ni
Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.
Kuhusu elimu ya Muungano wa Vijana,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi
za Kiserikali za pande Mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa
sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.
Amesema kwa sasa vijana wengi
wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali
zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu
Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.
Makamu wa Rais pia amehimiza makundi
mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wastaafu nchini waendelee na jitihada
zao katika kuelimisha umma ili kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya
jamii nzima na ya Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
DODOMA.
25-April-2017
No comments:
Post a Comment