Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa
kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume
wengi.
Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi
watamiminika kumtaka kimapenzi.
“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu
wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita akiwa
katika kipindi KTN nchini Kenya.
“Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu
wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”
Aliongeza, “Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi
kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata
Zari na kweli nimetulia,”
Muimbaji huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya
aliyekuwa mume wa Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini
kwa ugonjwa wa moyo.
No comments:
Post a Comment