Watafiti wameiboresha dawa ya sasa, Vancomycin kwa kutengeneza
aina nyingine ya dawa.
Vancomycin ilikuwa ikipoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria
aitwae enterococci ambaye husabisha madhara kwenye njia ya haja ndogo na
vidonda.
Aina mpya ya dawa hii ina nguvu mara elfu moja zaidi na
hushambulia vijidudu kwa njia tatu tofauti, kiasi cha vijidudu kushindwa
kupambana na dawa hiyo.
Inakadiriwa kuwa vijidudu vilivyokuwa vikipambana na dawa za antibiotics
husababisha vifo takriban elfu hamsini kila mwaka nchini Marekani na barani
Ulaya.
No comments:
Post a Comment