MKUU wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amekemea
vikali baadhi ya watu wanaoendelea kuwatumikisha watoto kwa kufanya kazi ngumu
na zenye ujira mdogo.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa kauli hiyo katika kilele cha sherehe ya
wafanyakazi Duniani, ambayo mkoani Geita imefanyaki katika viwanja vya CCM
Kalangalala Mjini humo, huku kitaifa maadhimisho hayo yakifanyika Mkoani
Kilimanjaro.
Kyunga alisema vitendo hivyo ni kinyume cha sheria, ambapo ameviagiza
vyombo husika ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali, viongozi wa dini, vyombo
vya dola na asasi zinazoshughulikia haki za watoto kushilikiana kwa dhati
kukomesha jambo hilo.
“Nitumie fursa hii lukemea baaadhi ya watu wanaowatumikisha watoto
kuwafanyisha kazi ngumu zenye ajira mdogo na usiokidhi haja zao, tunastahili
kushirikiana kupiga vita kwa nguvu zote…haki ya motto ni kupata elimu na
kulelewa katika mazingira bora na si vinginevyo,’’alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Pia RC Kyunga hakuacha kugusia suala la matumizi ya dawa za kulevya na
pombe haramu kwa wafanyakazi wote na wananchi, ambapo alipiga marufuk na kusema
si jambo zuri kwa matumizi ya madawa ya kulevya kwani zina athari kubwa kiakili,
kiafya na kuathiri ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment