Watu wataweza kuripoti uhalifu, kulipa faini na kupata taarifa
kwa kugusa kompyuta iliopo kifuani mwa roboti hiyo.
Taarifa inayokusunywa na roboti hiyo itasambazwa kwa maafisa wa
usafiri na trafiki.
Serikali inasema inalenga kuwa 25% ya kikosi chake kiwe ni cha
roboti kufikia 2030 lakini roboti hizo haziwezi kuichukua nafasi ya binaadamu.
"Nafasi za maafisa wa polisi hazitochukuliwa na mashine
hii," amesema Brigedia Khalid Al Razooqi, mkurugenzi mkuu wa huduma za
kisasa kielektroniki katika idara ya polisi Dubai.
"Lakini kutokana na kuongezeka idadi ya watu Dubai tunataka
tuwahamishe maafisa wa polisi ili wafanye kazi katika maeno yanayostahili na
waweze kushughulikia kikamilifu kuimarisha usalama mjini".
"Watu
wengi hufika katika vituo vya polisi au maeneo ya kuwahudumia wateja, lakini
kwa chombo hiki tunaweza kuufikia umma kila siku ya wiki."
"Roboti inaweza kuwalinda watu dhidi ya uhalifu kwasababu
inaweza kutangaza kinachotokea haraka moja kwa moja hadi katika kituo chetu
kikuu cha usimamizi."
Kwa sasa inaweza kuzungumza lugha ya kiarabu na kiingreza,
lakini kuna mipango ya kuongeza Kirusi, Kichina, Kifaransa na hata Ki Hispania
katika rekodi yake ya lugha.
Huenda roboti ya pili ikaanza kupiga doria mwaka ujao iwapo
ufadhili utapatikana, serikali ya Dubai imesema.
No comments:
Post a Comment