Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi
kumsifia hata kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii
kwani yeye na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa
Kanda ya Ziwa.
Musukuma anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza
ng'ombe za watu jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la
kujinufaisha wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa
wataziroga ng'ombe zote ili wanaokula ngo'mbe hizo Dar es Salaam wavimbe
matumbo.
"Napata shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya
ziwa labda tulikuja kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya
Ziwa hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa siku
tatu tukamatiwe ng'ombe kwa kisingizio kwamba ni ng'ombe za Wanyarwanda wakati
huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda wanawaambia toeni ng'ombe,
mnaenda kukamata ng'ombe za Wasukuma halafu unazipiga mnada na mnada wenyewe
unavyopigwa ni wa dili" alisisitiza Musukuma
Mbunge huyo aliendelea kuelezea namna watu wa Wizara ya
Maliasili wanavyofanya minada hiyo huku wakiwaumiza wafugaji
"Yaani ng'ombe 600 unaambiwa ulete milioni tatu halafu
wanatoa watu wao wa Ubungo sasa hapo nikupongeze kwa sababu gani? Tunajua
mipango inayoendelea kwenye wizara yako na niliwapigia kabisa watumishi wako,
wananiambia mliipenda wenyewe kwa kauli yake kama Mwenyekiti wa Chama kesho
yake akapiga ng'ombe za watu mnada yaani ng'ombe 500 zinauzwa milioni
tatu" alisema Musukuma
Joseph Msukuma aliendelea na msimamo wake
"Nataka nikwambie sisi Wasukuma sasa tumeamua na
ninazungumza uelewe tutaziroga hizo ng'ombe mtavimba matumbo mnaozila huko Dar
es Salaam, haiwezekani
kwanini wanunuzi watoke Dar es Salaam peke yake yaani leo siku ya mnada watu
wametoka na malori Pugu wamejuaje kama wanakuja kushinda kwenye minada.
Mnatukamatia ng'ombe hivi hii serikali imekosa sehemu ya kukusanya hela mpaka
mkanyang'anye ng'ombe za wafugaji haiwezekani Mh. Maghembe"
No comments:
Post a Comment