CHADEMA Kutoa Tamko Zito Leo - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 31 July 2017

CHADEMA Kutoa Tamko Zito Leo

Kamati Kuu ya CHADEMA   imekutana kwa siku mbili, tarehe 29 hadi 30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .

Taarifa iliyotolewa  jana  na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima.

Hata hivyo kikao hicho kilijadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua katika ajenda  ambapo ni pamoja na  kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo  taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leo  Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here