Serikali Kuunda Kamati ya Kukagua Viwanda Vyote Nchini - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 28 July 2017

Serikali Kuunda Kamati ya Kukagua Viwanda Vyote Nchini

Serikali  imeteua kamati maalumu yenye kushirikisha wataalamu pamoja na wakuu wa mikoa wa kila mkoa, itakayozunguka kukagua utendaji wa viwanda vilivyobinafsishwa, na kisha ndani ya siku 15 itatoa maamuzi.

Imesema viwanda watakavyoshughulika navyo ni vile vilivyobinafsishwa na ambavyo havifanyi kazi, lakini pia kuhakikisha uzalishaji wa kiwanda husika kama ndio ulioruhusiwa. 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema hayo jijini Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa wapo waliopewa viwanda kwa shilingi moja na wengine kwa Sh milioni 10, vingine vikifanya kazi, vingine vikiwa havifanyi kazi iliyokusudiwa na vingine kutokufanya kazi kabisa.

Alisema Kamati hiyo itafuatilia na tayari ameandika barua kwa wakuu wote wa mikoa nchini, na kupewa hadidu za rejea ili waweze kupitia kiwanda kimojakimoja kuhakikisha utendaji kazi wake. 

“Wakati Kamati hiyo ikikagua, wakikiona kiwanda wanapiga simu kwake na kwa msajili wa hazina ili kwenda kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi na baada ya hapo Augusti 15 watafanya maamuzi,”alisema.

Alisema yeyote aliyepewa kiwanda ni lazima kifanye kazi na kwamba kama anayehusika ameshindwa, atafute mtu mwingine ili kifanye kazi, la hasha ameagizwa akakichukue, kwani wapo watanzania ambao ni vijana wanatafuta kazi wakihitaji kutolewa vijiweni na kupewa viwanda waviendeshe na taasisi za kuwaelekeza zipo.

Alisema lengo la kubinafsisha viwanda ni ili vizalishe bidhaa ambazo zitatumika nchini na nyingine ziweze kuuzwa nje ya nchi na kuleta fedha za kigeni, vifanye kazi viweze kutoa ajira kwani asilimia 65 ya idadi ya watu nchini n I vijana na wengi wao hawana ajira.

“Kuna viwanda vilivyobinafsishwa na vinafanya kazi, hivyo hatuna shida navyo bali vile ambavyo havifanyi kazi, kwani malengo yetu ni wote wenye viwanda vifaye kazi hata vile vilivyosimama ili vikidhi malengo yaliyotakiwa,” alisema Mwijage na kuongeza kuwa viwanda vingi vilitolewa kwa Shilingi moja na vingine hadi Shilingi milioni 10.

Alitoa wito kwa wakuu wa mikoa, kukagua kiwanda kimoja baada ya kingine na hata kuhoji umiliki, hivyo mhusika anatakiwa kuwa na nyaraka stahiki, kwani ubinafsishaji dhamira yake kubwa ilikuwa ni kuwepo kwa ajira.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here