Mkali wa muziki wa Bongo Flava, Diamond ameeleza mambo machache kuhusu kolabo yake na rapper wa Marekani, Rick Ross.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Hallelujah’ ameiambia Coconut Fm kuwa ngoma hiyo ni yake Rick Ross kashirikishwa tu.
“Ni wimbo ni wangu mpya nimemshirikisha Rick Ross, kusema wimbo unaitwaje hiyo bado” amesema Diamond.
Katika hatua nyingine amezungumzia ngoma yake ‘Hallelujah’ aliyowashirikisha Morgan Heritage kwa kusema ngoma hiyo alikuwa ameshafanya verse moja na chorus, hivyo walichofanya kundi hilo ni kutuma verse yao tu na mchezo ukawa umeisha.
No comments:
Post a Comment