Usome Ushahidi Uliotolewa Mahakamani wa Kesi ya Lulu ya Kuua Bila Kukusudia - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 20 October 2017

Usome Ushahidi Uliotolewa Mahakamani wa Kesi ya Lulu ya Kuua Bila Kukusudia

         
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, imeendelea leo Oktoba 19 katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam ambapo upande wa mashtaka umeanza kuwasilisha ushahidi katika kesi hiyo.


Kesi hiyo ikiendelea mahakamani, mdogo wa marehemu Kanumba, Seth ambaye alikuwa akiishi na kaka yake na alikuwepo siku ya tukio, alitoa ushahidi kwa namna alivyoweza kushudia tukio zima lililopolekea kifo cha ndugu yake.

Akitoa ushahidi, Seth alisema, “Siku ya tukio marehemu Kanumba alinambia nisitoke nyumbani anataka tutoke wote kuanzia saa sita usiku, akaja Lulu na Kanumba ndiye aliyemfungulia mlango Lulu, alipofika ndani nikasikia akimuuliza Lulu kwanini anaongea na boyfriend wake mbele yake? Katika malumbano yao Kanumba alikuwa akimvuta Lulu arudi ndani na Lulu naye alikuwa anataka kutoka nje, wakati wakiendelea kugombana mlango wa chumba changu sikuufunga.”

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa, “Baada ya ugomvi Lulu alikuja chumbani kwangu akilia, akanambia Kanumba kadondoka amejaribu kummwagia maji haamki. Na ilikuwa mara ya kwanza kuona ugomvi kati yao, nilipoingia chumbani nilimkuta Kanumba chini kaegemea ukuta nikamlaza chali nikamtafuta daktari wake, Dk Kageiya, alipofika alimfanyia chek up akanambia ameshafariki ila akashauri tumpeleke Hospitali ya Taifa Muhimbili.”

Baada ya kutolewa kwa ushahidi huo wa upande wa mashtaka, kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Oktoba 20, 2017.

Steven Kanumba ambaye alikuwa mmoja wa waigizaji wakubwa nchini Tanzania na Afrika, alifariki dunia Aprili 7, 2012 akiwa nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here