KAMANDA Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ametoa ripoti ya matukio ya kihalifu yanayoendelea hapa nchini ambapo jeshi hilo linaendelea kupambana nayo usiku na mchana.
Tukio la kwanza ni kupatikana kwa silaha aina ya SMG, Bastola moja na risasi 17 pamoja na mabomu ya kijeshi.
Aidha kamanda Mambosasa amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata wahalifu sugu waliokuwa wakionekana eneo la Mbande, wakiwa na pikipiki ambayo haina namba, na baada ya kuona askari wanawafatilia walianza kuwamiminia risasi ili wasitishe zoezi hilo.
Jeshi la polisi halikuweza kurudi nyuma badala yake, lilijibu mapigo na kupambana na wahalifu hao, mpaka walipofanikiwa kuwashambulia vijana hao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 38 hadi 40, ambapo miili yao bado imehifadhiwa hospitali ya muhimbili.
Aidha Kamanda Mambosasa amewapongeza askari kwa juhudi zao, pia amesema juhudi za kuutafuta mtandao wa majambazi hao zinaendelea. Matukio mengine ni pamoja na wizi wa magari, laptop, simu za aina mbalimbali.
No comments:
Post a Comment