On the stage anafahamika kama Chris Brown, ila jina lake halisi ni Christopher Maurice Brown, alizaliwa Mei 5, 1989 Tappahannock- Marekani.
Chris alianza kupata umaarufu mwaka 2005 kupitia albamu yake ya kwanza ya ‘Chris Brown’ hii ndiyo albamu iliyofungua njia katikia maisha yake ya kimuziki.
Mwaka 2007 aliachia albamu yake ya ‘Exclusive’, kisa akaja na ‘Graffiti’ 2009, ‘F.A.M.E.’ ilitoka mwaka 2011 na 2012 alitoa ‘Fortune’, wakati albamu ya sita ya ‘X’ ikitoka 2014.
Albamu ya ushirikiano ya kati ya Chris Brown na rafiki yake Tyga ‘Fan of a Fan: The Album’ imetoka mwaka 2015, huku ‘Royalty’ ikifuatia mwaka huo huo 2015. Kwa sasa mashabiki wa msanii huyo wanangojea albamu ya tisa ya ‘Heartbreak on a Full Moon’ ifikapo Oktoba 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment