Producer Lamar ataja mastaa 10 Bongo waliotimba Fishcrab Auto Care - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 10 October 2017

Producer Lamar ataja mastaa 10 Bongo waliotimba Fishcrab Auto Care

Producer wa muziki Bongo kutoka studio za Fish Crab, Lamar ametaja mastaa wa Bongo waliopata huduma katika biashara yake mpya Fishcrab Auto Care ambayo anajihusisha na service za magari na Lamar ameeleza wazo nzima la kuanzisha kitu hicho na namna anavyokiendesha bila kuathiri maisha yake ya kimuziki.
Idea ya Fishcrab Auto Care
Mimi baada ya kufanya muziki nilianza kufanya kazi kampuni ya DAF ambao wanajihusisha na mambo ya magari, kwa hiyo nikapata experience nikasema kwanini nisifanyi kitu kama sehemu ya service kwa ajili ya kuwarahishia watu na kuweza kufanya usafi wa magari yao na nikapata sehemu hii hapa ndio nikawekeza.

Idea ilikuwepo kama miaka minne iliyopita, kwa sababu mimi na Jaffarai tulianza kutafuta eneo kwa ajili ya car wash yake, nikasema na mimi ngoja niangalie inaendaje halafu na nitakuja kufanya kitu changu.
Mastaa waliotimba Fishcrab Auto Care
Mastaa kama TID, Soudy Brown, Quick Rocka, Dj Venture, Bob Junior, Musa Hussein, Bill Nass, Dully Sykes, Perfect Crispin, Jaffarai, Mwasiti na wengineo wamekuja lakini bado wanaendelea kuja wanatoa support nzuri.
Kuitangaza zaidi kuliko muziki
Kitu kinapokuwa kipya lazima ukitangaze (hutangaza Instagram), watu wanajua mimi ni producer na nimeshafanya kazi na wasanii kibao.
Tuache muziki sasa tutangaze car wash kwa sababu muziki unajulikana kabisa ni passion yangu hata ukiniamsha usingizini na produce muziki, kwa hiyo najaribu kutangaza kitu ambacho nimewekeza pia.
Kuhusu muda wa studio
Studio unajua mtu anafanya booking, kwamba nataka kuja kurekodi, nataka kuja kufanya tangazo, kwa hiyo mtu ananipigia, najaribu kuwatengenezea mipango.
Mimi sasa hivi kwa siku nafanya kazi tatu; kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa tisa naingia DAF, nikitoka hiyo saa tisa nakuja huku car wash mpaka saa moja halafu naingia studio, ndio ipo hivyo.
Vipi kuajiri
Hadi sasa hivi nimeajiri vijana sita, ambao kuna watu wa kuosha wanne na watu wa service wawili.
Mimi muda mwingine naingia nafanya service, naosha magari siyo kwamba wao nimewaajiri mimi siwezi kufanya, no!!, naingia inapobidi kwa sababu muda mwingine kazi zinazidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here