Mtandao wa kijamii wa WhatsApp upo mbioni kuongeza sehemu mpya kwa watumiaji wake itakayomuwezesha mtumiaji kuonesha eneo alipo kwa muda huo (Live Location) kwa watu atakaowasiliana nao kupitia WhatsApp.
Haya ni maboresho ambayo mtandao huo umedhamilia kuyafanya kwa mwaka huu ili kuendana sawa na programu nyingine kama Snapchat, Facebook, iMessanger n.k .
Sehemu hiyo ya Live Location itakusaidia kuwaonesha marafiki, ndugu na jamaa zako sehemu uliyopo kwa dakika 15, hadi masaa 8 kutokana na wewe mwenyewe unavyotaka, lakini pia unaweza kuibadilisha kwa aidha uiweke Automatic au Manually kama ilivyo kwa mitandao mingine pindi unapotuma kitu.
Kupitia blog ya WhatsApp wamesema kuwa sehemu hiyo itakuja kwa watumiaji wote wa Android na iOS.
Hivi ndivyo utakavyotumia Live Location Shairing kwenye programu yako.
1- Ingia sehemu ya kuchat kama kawaida chagua jina au kundi unalotaka lijue sehemu uliyopo. Kisha bonyeza na chini ya jina lake au jina la kundi utaona sehemu imeandikwa ‘Live Location Share’ na utabonyeza hapo kuruhusu.
Kumbuka huduma hii bado haijaanza kufanya kazi na ikishaanza kupatika itakupasa u-update simu yako ili uweze kuanza kuitumia. WhatsApp wamesema sehemu hii itaanza kupatikana wiki chache zijazo. Je, maboresho hayo ya WhatsApp yatafanya mitandao mingine kama Snapchat kukosa watumiaji?
No comments:
Post a Comment