Polisi Yaua Majambazi Matano Kahama - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 6 November 2017

Polisi Yaua Majambazi Matano Kahama

Watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi waliokuwa doria.
Taarifa ya polisi imesema watu hao waliuawa walipojaribu kuwavamia wafanyabiashara wa madini katika machimbo ya Mwime nje kidogo ya Mji wa Kahama.

Watuhumiwa pia wanadaiwa kuhusika na mauaji ya viongozi wa Serikali ya Mtaa, polisi na wanasiasa mkoani Pwani katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema jana kwamba watu hao walijeruhiwa usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mwanva katika Halmashauri ya Mji wa Kahama walipokabiliana ana kwa ana na polisi waliofika eneo hilo.

Kamanda Haule alisema baada ya polisi kufika kwenye eneo la tukio, watu hao walijificha kwenye mashimo yanayotumiwa kuchimba mchanga na kuanza kurushiana risasi na askari.

Alisema katika mapambano hayo, watuhumiwa walizidiwa nguvu na kujeruhiwa na walifariki dunia walipokuwa njiani kupelekwa hospitali.

Alisema katika eneo la tukio, polisi walikuta bunduki moja aina ya SMG na risasi 25 zilizokuwa kwenye magazini. Pia walikuta mabomu mawili ya kutupa kwa mkono.

Katika uchunguzi wa awali, Kamanda Haule alidai kwamba watu hao ni miongoni mwa waliokuwa wakifanya uhalifu mkoani Pwani ambao walikimbia huko baada ya kudhibitiwa.

Kamanda Haule aliwataka wananchi kufika katika Hospitali ya Mji wa Kahama kuwatambua marehemu kauli ambayo pia ilitolewa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kahama, Dk David Lucas.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here