Mwendesha mashitaka huyo alisema
wanafamilia hao kupitia mwanga wa taa ya sola waliweza kuwatambua watuhumiwa
kabla wazazi hawajapelekwa Hospitali ya Misheni Chimala walikolazwa kwa ajili
ya matibabu.
Kutokana na makosa hayo Luchagula
aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu
wengine walio na tabia hizo wilayani hapa na kwingineko nchini.
Akito adhabu kwa washitakiwa,
Hakimu Mkasela alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na
pande zote mbili na kwamba kwa kosa la kwanza la unyangaji wa kutumia silaha
washitakiwa watakapaswa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kwa kosa la pili
la ubakaji watatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwao na watu
wengine.
Awali washitakiwa waliiomba
Mahakama kuwapunguzia adhabu wakisema bado umri wao ni mdogo na wanategemewa na
familia zao, maombi ambayo yalitupiliwa mbali na hakimu Mkasela.
No comments:
Post a Comment