
ASKARI tisa wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa mauaji ya
mkazi mmoja wa Kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora.
Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi, Samson Kabigi, alisoma mashtaka dhidi ya watuhumiwa
hao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Agatha
Chigulu.
Alidai kuwa askari hao wote
wa Kikosi cha 823 Msange, walitenda kosa hilo Septemba 10, mwaka huu.
Inadaiwa kuwa askari hao
waliwashambulia wananchi mjini Tabora baada ya mkesha wa
Fiesta.
Askari hao ni MT
109535 Koplo Msafiri Kitwima (26) na MT 92697 Private Thobias Salum (30) wakazi
wa Kata ya Chem Chem, MT 114612 Private Shomary Hemed (24), MT
114685 Private Yusuph Muluthary (25) na MT 114110 Private Rajab Mbasa (24).
Wengine ni MT 114142 Private
Selestine Machemba (24), MT 114125 Private Said Rashid (27), MT 114118 Private
Rogasian Shayo (24) na MT 114684 Private Yustin Mwingira (24), ambao
wote ni wakazi wa Kikosi cha 823 Msange.
Mwendesha Mashtaka Kabigi, alidai
washtakiwa wote kwa pamoja Septemba 10, mwaka huu saa 9.00 mchana walimuua
Omary Shaban.
Washtakiwa hawakutakiwa
kujibu chochote kwa vile shauri lao litasikilizwa na Mahakama
Kuu. Walirudishwa makabusu hadi Oktoba 5, mwaka huu kesi hiyo
itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment