Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights
Watch limeituhumu Kenya pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa
linalowashughulikia wakimbizi (UNHCR) kwa kutofuata sheria katika kuwarejesha
wakimbizi Somalia.
Shirika hilo, kwenye ripoti yake
iliyotolewa leo, limesema Kenya haiwapi wakimbizi fursa ya kuamua iwapo
wanataka kusalia kambini Dadaab au kurejea Somalia.
Mkurugenzi wa masuala ya haki
katika Human Rights Watch Bill Frelick amesema UNHCR haitawapa wakimbizi habari
sahihi kuhusu hali halisi ya usalama Somalia.
Serikali za Kenya na Somalia
zimesema wakati umefika wa kufunga kambi hizo.
Kenya ilikuwa imetangaza kwamba
kambi ya Dadaab itafungwa kufikia mwezi Novemba.
Shirika la Human Rights Watch
linasema kunao baadhi ya wakimbizi ambao wameamua kuondoka kambini wakihofia
kuondolewa kwa lazima mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment