Ghasia zilizuka kwa usiku wa pili
baada ya kuuawa Keith Lamont Scott kwa kupigwa risasi na afisa mweusi Jumanne.
Muandamanaji mmoja yupo katika hali
mahututi baada ya kuzuka ufyetulianaji risasi baina ya raia, maafisa wa mji
walisema.
Bwana Scott was ni mwanamume wa
tatu raia wa Marekani mwenye asili ya kiafrika kuuawa na polisi katika wiki
moja.
Mauaji haya yamesbabisha maandamano
makubwa katika siku za hivi karibuni
Polisi ya kupmabana na fujo imetumia gesi ya kutoa
machozi walipokabiliana na mamia ya waandamanj. Idara ya polisi inasema maafisa
wake wanne wamejeruhiwa.
Awali Gavana wa North Carolina
Governor Pat McCrory amesema ameanzisha jitihada kutuma jeshi la ulinzi na
maafisa wa polisi wa trafiki kusaidia kukabiliana na maandamano hayo.
"ghasia zozote zinazoelekezwa
dhidi ya raia wetu au maafisa wa polisi au kusababisha uharibifu wa mali
hazikubaliki," alisema.
Waandamanji wana hasira kuwa bwana
Scott, mwenye umri wa miaka 43, ameuawa na Polisi Jumanne mchana katika hali ya
kutatanisha karibu na eneo la makaazi.
No comments:
Post a Comment