Kampuni ya Microsoft imeshtumiwa na kundi la haki za
wateja la Consumer Rights dhidi ya programu yake ya Windows 10.
Kundi hilo limesema limepokea mamia
ya malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa programu hiyo .
Watumiaji wa programu hiyo
wanalazimika kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na faili kupotea.
Hatahivyo Microsoft ilitetea
programu hiyo ya Windows 10 na kusisitiza kuwa imekuwa ikitoa usaidizi kupitia
mtandaoni na vilevile kwa simu.
Imeongezea kwamba itawasaidia watu
kupata programu yenye manufaa na yenye usalama dhabiti, kulingana na msemaji wa
kampuni hiyo.
Kundi hio limesema watumiaji wamekuwa wakilalamikia
ujumbe uliokuwa ukijitokeza kwenye tarakilishi na simu zao kila mara,
kuwahimiza kuboresha programu hiyo mbali na programu hiyo ya Windows 10
kujiweka yenyewe bila idhini ya mtumiaji.
Pia kumekuwa na malalamiko
kuhusiana na huduma mbaya kwa wateja wake,pale wanapohitaji msaada kutoka kwa
kampuni hiyo.
Programu hiyo ya windows 10
ilizinduliwa mwezi Julai mwaka 2015, na hutumika katika tarakilishi,simu aina
ya smartphone, na vifaa vya kusikilizia sauti vya HoloLens.
No comments:
Post a Comment