Rais mstaafu, Jakaya Kikwete
ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi
ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Kikwete amesema uamuzi huo ni wa
busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia
tatizo hilo.
Kikwete aliyemtumia salamu za pole
Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema misaada ya haraka na dharura
inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za
kibinadamu.
Kiongozi huyo mstaafu ameyasema
hayo katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za watumishi wa afya, 10
zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya
Benjamin Mkapa mkoani Pwani.
“Ndugu zangu pamoja na leo hii
tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani kwetu, naomba tusimame
tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na
pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.
Ameongeza kuwa: “kiukweli
amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa
haya.”
Hafla ya makabidhiano hayo
imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.

No comments:
Post a Comment