Wanasayansi waliripoti mara ya kwanza kuhusu kuwepo kwa maji
katika mwezi huo kwa jina Europa mwaka 2013 baada ya kuufuatilia kwa karibu kwa
kutumia darubini kwa jina Hubble.
Sasa, wamethibitisha hilo baada ya kuitumia Hubble kuchunguza
mwezi huo ulipokuwa unapita mbele ya sayari ya Jupiter (Zohali).
Walitumia darubini hiyo kuchunguza nguvu za mionzi ya jua kuona
ikiwa ilikuwa inamezwa na kitu chochote kutoka kwa mwezi huo.
Walichunguza mara kumi, na mara tatu wakafuailia kilichoonekana
kama "vidole vyeusi' vilivyokuwa vikitoka kwa Europa.
Mtaalamu aliyeongoza uchunguzi huo William Sparks, anasema
hawezi kufikiria kitu kingine kinachoweza kusababisha jambo kama hilo kando na
maji.
Michirizi hiyo ya inayoaminika kuwa ni ya maji ilionekana eneo
ambalo miaka kadha iliyopita, wanasayansi waliokuwa wakitumia Hubble,
waligundua oksijeni na haidrojeni, viungo vinavyounda maji.
Ni hatua muhimu kwa sababu Europa, sehemu yake kubwa imefunikwa
na bahari ya maji, na ni moja ya maeneo ambayo inaaminika huenda kukawa na
viumbe wanaoishi anga za juu kando na dunia.
Wanasayansi wanakadiria kwamba huenda wakaweza kuchota maji hayo
na kuyafanyia uchunguzi kwa kupitisha chombo cha anga za juu kwenye michirizi
hiyo.
Njia nyingine, ambayo inausisha kupeleka chombo ambacho kitatua
katika mwezi huo na kuchimba kilomita nyingi ndani ya barafu ili kufikia maji,
huenda ikawa na changamoto nyingi sana.
Michirizi ya maji imewahi kuonekana katika mwezi wa
Enceladus, mwezi wenye barafu wa sayari ya Saturn (Sarteni).
Chombo cha anga za juu cha Cassini
kwa sasa kinazunguka sayari hiyo na tayari kimepitia katika michirizi hiyo
kufanya uchunguzi.
Hata hivyo, vifaa vya chombo hicho
havina uwezo wa kuchunguza uwepo wa viumbe hai.
No comments:
Post a Comment