
Wizara ya
elimu, Sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi imezifuta shule za awali, msingi
na sekondari nchini zaidi ya 40 ambazo hazijasajiliwa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Usajili wa shule katika wizara hiyo, Khadija Mcheka, alisema Mei
mwaka huu baada kuzipa miezi miwili shule ambazo hazijasajiliwa kufanya hivyo,
walizifungia shule nyingine 12.
Shule
zilizofungiwa kwa kuendesha shughuli zake bila usajili zilitajwa kuwa ni shule
za awali na msingi za Must Lead ya mkoa wa Pwani, na za mkoa wa Dar es Salaam
ni Brainstorm, Pax, Lassana, Grace, Rose Land, Julius Raymod, St Thomas, Mary
Mother of Mercy, Noble Sinkonde, Immaculate Heart of Mary, St Columba, Corner
stone, Dancraig, Mwalimu Edward Kalunga, Edson Mwidunda, Gisela, Kingstar, St
Columba awali, Bilal Muslim, Thado, Hocet , Elishadai, Lawrance Citizen,
Comrade, Dar Elite Preparatory na Golden Hill Academy na Hekima.
Nyingine ni
Pwani Islamic, St Kizito na Rwazi Encysloped za Kagera, Dancraig na Qunu za
Pwani, Hellen’s ya Njombe, Joseph ya Arusha, Samandito na Maguzu za Geita.
Alizitaja shule za Sekondari zilizofungiwa kwa sababu hiyo kuwa ni Hananasif,
Elu, Hocet, Safina za Dar es Salaam na Namnyaki ya Iringa.
“Baada ya kutoa
tangazo kutokana na kubaini kuwapo shule nyingi zisizosajiliwa, wapo
waliojitokeza na nyingine tumezifungia kutokana na kutokidhi viwango vya usajili
lakini pia tunaamini wapo waliojificha wakiendelea kutoa huduma,” alisema Mcheka.
Aliwaagiza
wakaguzi katika kanda na wilaya, kufanya ukaguzi na kutoa taarifa kwa zile
ambazo hazijafungiwa na ikithibitika hazijasajiliwa, kuzifungia mara moja.
No comments:
Post a Comment