
Hofu ya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya
uchochezi, imetoweka baada ya mahakama hiyo kukubaliana na utetezi wa
wadhamini wake kuwa, Lissu yupo Ujerumani kwa matibabu.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, alishindwa kuhudhuria mahakamani siku ya juzi na hivyo wadhamini wake kutakiwa kufika mahakamani jana kujieleza, kwanini mtuhumiwa huyo asifutiwe dhamana.
Kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu ni kesi Na. 208 katika gazeti la MAWIO akiwa ni mtuhumiwa namba nne sambamba na Jabir Idrissa, Simon Mkina, na Ismail Merhaboob.
Jabir ni mwandishi mwandamizi wa MAWIO, Mkina ni mhariri wa gazeti hilo na Merhaboob ni meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti inayojulikana kwa jina la Flint.
Jana, wadhamini wa Lissu Ibrahim
Ahmed na Robert Katula walisimama mbele ya Hakimu Thomas Simba anayesimamia
kesi hiyo, na kusema kuwa Lissu hakutokea mahakamani kwa sababu amesafiri
nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, upande wa mashitaka
ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kisheruji uliiomba
mahakama kuzuia hati ya kusafiria ya mshitakiwa Lissu pamoja na kumuwekea
sharti la kuiomba mahakama kibali cha kusafiria endapo atarudia tena kosa hilo
kutokana kwamba hakufuata sheria kwa sababu alitakiwa kutoa taarifa mapema
kabla ya siku ya shtaka kusikilizwa.
Lakini Hoja hiyo ilipingwa na
Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala na kuiomba mahakama kutenga siku
nyingine ambapo alimuahidi hakimu kuwa kosa hilo halitajirudia tena na siku
husika ya kusikilizwa shitaka mshatikiwa atakuja mahakamani.
Baada ya kusikiliza maombi ya pande
zote mbili, Hakimu Simba alitoa onyo kali kwa mshitakiwa na kuwaambia wadhamini
wa Lissu kuwa, endapo siku nyingi mshitakiwa huyo hatakuja mahakamani,
wadhamini watalipa dhamana.
Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo
hadi Oktoba, 4, 2016 baada ya mawakili wa pande zote mbili kuiridhia tarehe
hiyo iwe siku ya kusikilizwa shtaka hilo.
No comments:
Post a Comment