Vyanzo vingine vya habari vinasema
watu waliouawa ni 40.
Ofisi ya Rais wa nchi hiyo Joseph
Kabila imepinga taarifa hizo, huku ikiwalaaumu viongozi wa maandamano hayo kwa
kuchochea ghasia hizo za umwagaji damu.
Upinzani nchini humo wamevilaumu
vyombo vya usalama kwa kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakiandamana kwa
amani juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo.
Wanaamini kuwa Rais Kabila anajaribu
kung'ang'ania madaraka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake.
No comments:
Post a Comment