Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza na watendaji katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Hermani
Kapufi,amewaagiza maafisa watendaji wa kata,vijiji na vitongoji
kushughulika na wale wote ambao watabainika wamewapatia ujauzito wanafunzi
ambao bado wapo masomoni.
Kauli hiyo ,ameisema wakati alipokutana
na watendaji katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya Wilaya ya Geita ambacho kilikuwa kimelenga kutatua changamoto za
watendaji wa kata,vijiji na vitongoji.
Amesema kuwa suala la baadhi ya watu
kuendelea kuwapa mimba watoto wa shule limekuwa ni changamoto ambayo
imesababisha kukatisha ndoto za baadhi ya wanafunzi kwa kuwashawishi kwa vitu
vidogo na mwisho wa siku kuwapotezea ndoto zao pamoja na mlengo waliyojiwekea.
“Natambua kuwa kuna tatizo kubwa
linaloendelea kwa maeneo ya hapa wilayani kwa watu kuendelea kuwapa mimba
wanafunzi na mwisho wa siku hakuna sheria yoyote inayochukuliwa mimi nikiwa
kama Mkuu wa wilaya hii ninawaagiza watendaji wote kuwashughulikia wale wote
ambao wanatabia ya namna hiyo serikali inawekeza fedha nyingi sana kwa
wanafunzi leo hii wanatokea baadhi ya watu kukatisha ndoto zao kamwe hatuwezi
kuwafumbia macho watu wenye tabia za namna hiyo”alisema Kapufi.
Aidha kwa upande wao watendaji
wamesema kuwa matatizo ya baadhi ya watu kuwapa mimba wanafunzi yapo mengi sana
katika maeneo wanayo yaongoza na kutokana na agizo hilo wanaamini kuwa wataweza
kuwaadhibu wale ambao wamekuwa na tabia za namna hiyo.
No comments:
Post a Comment