Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia
Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na
changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
“Ni wazi kwamba umri wake na hali
ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza
kulinusuru taifa hilo,”.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo
tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo
kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe
umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana
ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka
afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu
viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.
No comments:
Post a Comment