Rapper Kid Cudi kutoka Good Music amejitoa kwenye kuigiza show kubwa ya
TV ‘Empire’ siku chache kabla ya msimu wa tatu kuanza kuoneshwa.
Watayarishaji wa show hii wanasema Kid amejiondoa baada ya kutofautiana
na waandaji katika masuala ya ubunifu wa uhusika wake. Nafasi ya Kid Cudi
imeshachukuliwa na mtoto wa Master P, Romeo Miller maarufu kama Lil Romeo.
Romeo atakuwa akijulikana kama Gram ambaye ni mpenzi mpya wa Tiana na
pia atakuwa hasimu mkubwa wa rapa Hakeem.
Kid Cudi tayari
alikuwa amesharekodi baadhi ya vipande vyake na ameshaonekana kwenye trailer ya
show ya msimu wa tatu.
No comments:
Post a Comment