Wanadiplomasia wa Afrika kusini wamearifu umoja wa mataifa juu
ya uamuzi huo na kuilaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.
Uamuzi wa Afrika kusini kujiondoa ulitokana na shinikizo
ilikumbana nazo mwaka uliopita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir
wakati wa mkutano wa muungano wa nchi za Afrika mjini Johannesburg.
Septemba mwaka jana, mahakama nchini nchini Afrika Kusini
iliinyima serikali ya nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa
kukosa kumkamata Bw Bashir alipohudhuria kongamano hilo mwezi Juni mwaka 2015.
Serikali ilitaka kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema
Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.
Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi
kufanikisha chochote.
Aliongeza kuwa Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma
uliounda mahakama hiyo, na kwamba mkataba huo unabatilisha sheria zozote ambazo
huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa.
Kiongozi huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki
na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.
Kiongozi huyo aliyechukua mamlaka
kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 amekanusha madai hayo.
No comments:
Post a Comment