Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya
Saa 13:00hrs Katika Eneo La Buswelu Kata Ya Buswelu Wilaya Ya Ilemela Jiji Na
Mkoa Wa Mwanza, Askari Wakiwa Katika Misako Na Doria Walifanikiwa Kuwakamata
Watu Sita Wakiwa Na Silaha Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Pamoja Na Risasi
Ishirini Na Tatu, Ambazo Walikuwa Wakizitumia Katika Matukio Ya Unyang’anyi Wa
Mali Na Uporaji Hapa Jijini Mwanza Na Mikoa Mingine.
Aidha Tukio Hilo Limefanikiwa Baada
Ya Kupokea Taarifa Kutoka Kwa Raia Wema Kuhusu Uwepo Wa Wahalifu Hao, Ndipo
Askari Walifanikiwa Kumkamata Kwanza Jeremiah Maligia @ Mkumbo Miaka 25,
Mnyiramba, Fundi Seremala Mkazi Wa Malega – Singida Ambaye Alipohojiwa Alikiri
Kuhusika Na Kutaja Wenzake Waliokuwa Wakishirikiana, Na Kuwa Silaha Wamezificha
Kwa Mganga Wa Kienyeji Aitwaye Leornad Litta @ Makai Anayeishi Mtaa Wa Kagida –
Buswelu.
Askari Walikwenda Mahali Hapo Na
Kufanikiwa Kumkamata Mganga Huyo Wa Kienyeji Bwana Leornad Litta Miaka 39,
Akiwa Na Silaha Hizo Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Hapo Nyumbani Kwake
Na Risasi Ishirini Na Mbili Zinazotumiwa Na Bunduki Ya Aina Ya Short Gun Na
Risasi Moja Ya Rifle Aina Ya Mark Iv.
Aidha Katika Kuhojiwa Zaidi
Na Askari Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Waliwataja Washirika Wao Wanne Ambao
Walikuwa Wakishirikiana Katika Kufanya Uhalifu Ambapo Askari Walifanikiwa
Kuwakamata, Ambao Ni 1. Kamgisha Jovini Kamhambwa Miaka 40, Mlinzi Na Mkazi Wa
Iloganzala, 2. Juma Yusuph @ Jimi Miaka 35, Mkazi Wa Bwani Kinondoni, 3.
Samweli Peter Miaka 36, Mkazi Wa Busweli Na 4. Shabani Hussein Miaka 26, Fundi
Viatu Na Mkazi Wa Nyasaka Msumbiji.
Watuhumiwa Wote Walipofanyiwa
Mahojiano Walikiri Kwamba Silaha Hizo Walizitumia Katika Unyang’anyi Wa Mali Na
Uporaji Katika Maeneo Ya Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Aidha Jeshi La Polisi Kwa Sasa
Linaendelea Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo Na Matukio Waliyokuwa
Wameyafanya, Pindi Uchunguzi Ukikamilika Watuhumiwa Wote Watafikishwa
Mahakamani.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza
Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa
Wa Mwanza Akiwataka Kuendelea Na Tabia Ya Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Lao La
Polisi, Ili Tuweze Kudhibiti Uhalifu Katika Mkoa Wetu., Lakini Pia Anatoa
Angalizo Kwa Wananchi Haswa Vijana Akiwataka Kuacha
Tabia Ya Kujihusisha Na Uhalifu
Bali Wajikite Katika Kufanya Shughuli Halali Za Maendeleo, Kwani Jeshi La
Polisi Lipo Vizuri
Kuhakikisha Ulinzi Na Usalama Upo
Kwa Raia Wote Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza.
Katika Tukio La
Pili
Mnamo Tarehe 18.10.2016 Majira Ya
Saa 14:00hrs Mchana Katika Eneo La Ilemela Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa
Mwanza, Askari Walifanikiwa Kuwakamata Watu Wawili Ambao Ni 1. Rahim Feka Miaka
28, Mkazi Wa Ilala – Dar Es Salaam, 2. Ally Kawalale Miaka 32, Mkazi Wa
Jetrumo – Arport Dar Es Salaam, Wakiwa Wanataka Kuuza Gari Lenye Namba T.778
Azv Aina Ya Toyota Land Cruiser Lililokuwa Wameliiba Huko Ilala Jijini Dar Es
Salaam.
Aidha Watuhumiwa Hao
Walikamatwa Baada Ya Kupokelewa Taarifa Ya Kuibiwa Kwa Gari Hilo Huko Dar
Es Salaam Na Kwamba Kuna Uwezekano Kuwepo Eneo La Kanda Ya Ziwa, Ndipo
Ulifanyika Upelelzi Kuhusiana Na Taarifa Hiyo, Na Kufanikiwa Kuwakamata Watuhumiwa
Tajwa Hapo Juu Wakiwa Na Gari Hilo.
Watuhumiwa Wote Wapo Chini Ya
Ulinzi Wa Jeshi La Polisi Wakiendelea Na Mahojiano , Huku Taratibu Za
Kuwasafirisha Kwenda Dar Es Salaam Wakiwa Chini Ya Ulinzi Wa Askari
Polisi Zikiwa Bado Zinaendelea.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza
Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Rai Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa
Mwanza Akiwataka Kuacha Tabia Ya Kununua Vitu Vya Wizi, Bali Pindi Wanapoona
Biashara Za Wizi Zinataka Kufanyika Au Zinafanyika Watoe Taarifa Polisi Ili
Watuhumiwa Waweze Kukamatwa Na Kufikishwa Mahakamani.
Katika Tukio La
Tatu
Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya
Saa 23:00hrs Katika Kitongoji Cha Ibungiro Kijiji Cha Sagani Kata Ya Kandawe
Wilaya Ya Magu Mkoa Wa Mwanza, Mtu Mmoja Msichana Aliyejulikana Kwa Jina La
Dema Charles @ Bulayi Miaka 20, Mkazi Wa Kandawe, Ameuawa Kwa Kukatwa Na Vitu
Vyenye Ncha Kali Sehemu Za Kichwani Na Kiunoni
Akiwa Amelalala Na Watu
Wasiojulikana, Huku Wenzake Wa Wili Wakijeruhiwa Sehemu Mbalimbali Za Miili
Yao.
Majeruhi Waliojeruhiwa Katika Tukio
Hilo Ni 1.mariam Lucas @ Kapele Miaka 26, Mkazi Wa Kijiji Cha Sagani
Aliyejeruhiwa Shingoni Na Kwenye Kiganja Cha Mkono Wa Kulia, 2. Kapelele
Makubi @ Salulo Miaka 90, Ambaye Ni Baba Mwenye Nyumba/ Mji, Aliyejeruhiwa Mgongoni,
Kichwani Na Kiunoni.
Inadaiwa Kuwa Wauaji Hao Walifika
Katika Nyumba Hiyo Majira Tajwa Hapo Juu Na Kuwakuta Wenye Mji Wakiwa
Wamelala, Ndipo Waliingia Ndani Na Kufanya Mauaji Hayo, Hadi Sasa Hakuna Mtu
Yeyote Aliyekamatwa Kuhusiana Na Tukio Hilo.
Aidha Uchunguzi Wa Awali
Umebainisha Kuwa Mauji Hayo Yametokana Na Kulipiza Kisasi, Jeshi La Polisi Kwa
Sasa Lipo Katika Upelezi Pamoja Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo, Majeruhi
Wapo Katika Hospitali Ya Wilaya Ya Magu Wakiendelea Kupatiwa Matibabu Na Hali
Zao Zinaendelea Vizuri.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza
Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa
Wa Mwanza Akiwataka Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi La Polisi Ili Watuhumiwa Wa
Mauaji Hayo Wawezwe Kukamatwa Na Kufikishwa Katika Vyombo Vya Sheria.
Imetolewa Na:
Dcp: Ahmed Msangi
Kamanda Wa Polisi
(M) Mwanza
No comments:
Post a Comment