Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez amekabidhiwa kiatu cha
Dhahabu (European Golden Shoe) kwa kuibuka mfungaji bora Barani Ulaya msimu wa
2015/2016.
Suarez
alifunga magoli 40 katika La Liga , na hivyo kumfanya achukue kiatu hicho kwa
mara ya pili. Mara ya kwanza alichukua akiwa Liverpool msimu wa 2013/2014
Kiatu hicho hupewa mchezaji
aliyefunga magoli mengi katika ligi kuliko mchezaji mwingine yoyote kwenye ligi
kubwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment