BABA mmoja mkazi wa Kijiji cha Maji
ya Moto, Wilaya ya Arumeru mkoani hapa, Wilfred Kivuyo amemuua mtoto wake baada
ya kumchoma kisu tumboni, kwa kosa la kufungulia redio kwa sauti ya juu.
Kabla ya tukio hilo inadaiwa
yalitokea mabishano ya kugombea kupunguza sauti ya redio kati ya baba na mtoto,
ambapo baba aliamua kumchoma kisu tumboni mtoto wake na utumbo kutoka nje.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Charles Mkumbo alisema, tukio hilo lilitokea Oktoba 23, mwaka huu saa tatu
usiku katika Kijiji cha Maji Moto na kumtaja marehemu kuwa ni Abraham Wilfred
(22), ambaye kabla ya mauti alikuwa nyumbani akiendelea na shughuli zake huku
akiwa amefungulia redio.
Alisema siku ya tukio mtuhumiwa
huyo alifika nyumbani akiwa amelewa na kumkuta mtoto wake amefungulia redio kwa
sauti ya juu, ambapo alimtaka kupunguza sauti hiyo lakini mtoto huyo aligoma.
“Baada ya hapo mabishano na
kutoelewana kulijitokeza baina yao wakaanza kupigana, baba alipozidiwa nguvu na
mtoto wake alichomoa kisu cha kukunja kwenye mfuko wa suruali kisha akamchoma
tumboni na kumsababisha utumbo kutoka nje.
“Mara baada ya tukio hilo mtoto
huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa
ajili ya matibabu, lakini hata hivyo alifariki wakati madaktari wakiendelea
kuokoa maisha yake,” alisema Kamanda Mkumbo.
Kamanda Mkumbo alisema Jeshi la
Polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo ambaye baada ya tukio alikimbia ili
hatua zaidi za kisheria zisichukuliwe dhidi yake
No comments:
Post a Comment