Sakata la posho za madiwani wa Jiji
la Arusha bado halijapoa, baada ya Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini
kuliibulia katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),
akisema linakwamisha ukusanyaji wa mapato.
Sakata hilo liliibuka jana wakati
kamati hiyo ilipokuwa ikipitia na kuhoji hesabu za halmashauri hiyo kwa mwaka
wa fedha 2014/2015.
Mbunge huyo alisema halmashauri
hiyo imekata posho kwa madiwani na watendaji na kuzipeleka fedha hizo kwa
walimu, jambo ambalo linawavunja moyo wawakilishi hao wa wananchi kutimiza
majukumu yao.
“Madiwani ndiyo wanawasaidia
kuwahamasisha wananchi katika ukusanyaji wa mapato na hao mnawavunja moyo.
Mkurugenzi hamuwezi kufikia malengo kama mtakuwa watendaji peke yenu,”alisema
Selasini.
Alisema halmashauri hiyo ikimaliza
mvutano huo inaweza kuongeza mapato kutoka Sh12 bilioni hadi Sh18 bilioni na
kujiendesha bila kutegemea ruzuku.
Mbunge huyo alisema katika
halmashauri zote nchini hakuna diwani anayelipwa posho ya Sh10,000, kwa nini
madiwani wa jiji hilo pekee walipwe kiasi hicho.
Akijibu hoja hiyo, mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Athuman Kihamia alisema hakuna diwani anayelipwa kiasi hicho
cha fedha na kwamba, madiwani wote wanalipwa posho ya Sh40,000 kwa mwezi na nauli
Sh10,000 kulingana na kanuni walizokubaliana mwaka 2003.
Alisema madiwani hao walikuwa na
posho zipatazo tano ambazo ni nauli, kujikimu, vikao, madaraka na mawasiliano.
Pia, Kihamia alisema walikuwa wakilipwa Sh150,000 za mafuta kinyume na kanuni walizokubali kuzitumia za mwaka huo.
Pia, Kihamia alisema walikuwa wakilipwa Sh150,000 za mafuta kinyume na kanuni walizokubali kuzitumia za mwaka huo.
“Siwezi kurudia makosa kwa kulipa
fedha zisizofuata kanuni na utaratibu, maana mtakuja kunihoji hapa kwa nini
nimezilipa,” alisema.
Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas
Malocha alimpongeza mkurugenzi huyo kwa kufuata misingi na utaratibu wa kanuni
na sheria katika uendeshaji wa jiji hilo.
Akizungumza nje ya kamati
hiyo, Meya wa jiji hilo, Calist Lazaro alitaka liachwe lijiendeshe lenyewe bila
kuingiliwa.
No comments:
Post a Comment