Taifa la Burundi hatimaye limekuwa taifa la kwanza kujiondoa rasmi
katika mkataba wa Roma unaosimamia mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa
kivita ICC.
Hatua
hiyo inajiri baada ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kutia saini sheria
iliopitishwa na bunge pamoja na seneti ya kuiondoa Burundi katika mkataba huo.
Wiki iliopita ,bunge la Burundi
liliidhinisha mpango wa baraza la mawaziri kukata uhusiano na mahakama hiyo ya
mjini Hague.
Tayari mahakama ya ICC imeitaja mipango ya Burundi ya kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kuwa ‘pigo’ katika vita dhidi ya watu wasioheshimu sheria.
Tayari mahakama ya ICC imeitaja mipango ya Burundi ya kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kuwa ‘pigo’ katika vita dhidi ya watu wasioheshimu sheria.
Barua iliotiwa saini na rais
Nkurunziza kuiondoa Burundi katika ICC
Mwendesha mashtaka wa ICC
alinukuliwa akisema kuwa atachunguza kile kilichotokea Burundi wakati wa
maandamano dhidi ya rais Pierre Nkurunziza.
Aliyekuwa waziri wa haki nchini
Senegal Sidiki Kaba,ambaye anaongoza bodi hiyo ya ICC ,alitoa wito kwa Burundi
kuzungumzia wasiwasi wake badala ya kujiondoa katika mahakama hiyo.
Mwaka uliopita,marais wa Umoja wa
Afrika walipitisha pendekezo kutafuta njia ambayo bara la Afrika lingeweza
kujiondoa katika mahakama hiyo kwa pamoja.
Kumekuwa na malalamishi kwamba
mahakama hiyo inalenga maswala ya Afrika pekee.
Kesi zote zinazoangaziwa na mahakama hiyo zinatoka Afrika.
Kesi zote zinazoangaziwa na mahakama hiyo zinatoka Afrika.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment