Mchezaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ureno anaye chezea klabu ya
Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo baada ya kufanya mahojiano na jarida
la Coach Magazine na kufunguka mambo kadhaa kuhusu soka, katika interview hiyo
Ronaldo kazungumza alichojifunza katika soka na kamuongelea mpinzani wake
Lionel Messi pamoja na beki Ashley Cole.
Qn.
Kitu gani kikubwa ambacho mchezo wa mpira wa miguu umekufunza?
Ans. Kutumia mawazo hasi ya watu
wanaokupiga kukuhamasisha, kiukweli nawahitaji haters kwa sababu wamenisaidia
kufanikisha kila kitu nilichofanikiwa.
Qn. Kuhusu Lionel Messi?
Ans. Kuna heshima kubwa sana kati
yangu na Lionel Messi, lakini vyombo vya habari vinapenda tuonekane kama
tunaupinzani mkubwa sana lakini hatuna upinzani huo, haina maana kama sisi ni
marafiki wa karibu sana lakini kuna heshima kubwa kati yetu
Qn. Ni beki gani mgumu ambaye
amekuwa akikupa wakati mgumu
Ans. Ashley Cole ndio beki mgumu sana
kumpita niliyewahi kukutana nae.
Cole na CR7 wameshakutana kuanzia
kwenye ngazi ya taifa mpaka kwenye vilabu, wakati CR7 akiwa Old Trafford na
Cole akiwa Gunners na baadae The Blues.
No comments:
Post a Comment