Rais mstaafu kutoka kwenye awamu ya
nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kujibu
kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni.
Usiku wa kuamkia leo, kupitia
akaunti yake ya Twitter, Rais Mstaafu wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete aliandika
masikitiko yake juu ya namna watu wanavyotumia picha zake na kupotosha yale
aliyoyasema juzi akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kufanikisha
matwaka yao ya kisiasa.
Nimestaafu naomba niachwe nipumzike. Nisingependwa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya Serikali. Namuunga mkono Rais na Serikali yake.
Nasikitishwa sana na matumizi
mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka
kutimiza malengo yao ya kisiasa.
Aidha, Rais Kikwete aliwataka watu
hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa
kupumzika.
Rais Kikwete pia alikanusha tuhuma
za kuwa anatofauti na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa
anamuunga mkono Rais Magufuli pamoja na serikali yake.
Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa.
Nimestaafu naomba niachwe
nipumzike. Nisingependwa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya Serikali.
Namuunga mkono Rais na Serikali yake.
Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete
ambayo imekuwa ikipotoshwa mtandaoni ni ile aliyoitoa kwenye maadhimisho
ya miaka 55 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo aliwataka viongozi
wapya kuenzi mazuri ya nyuma akimaanisha kwamba hivi sasa yeye ndo Mkuu wa Chuo
hicho(Chancellor), hivyo akaahidi kuyaenzi mazuri aliyoyakuta toka kwa
watangulizi wake
“Ukiwa mpya lazima watu waone una
mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo," alisema Rais
Mstaafu Kikwete na kuongeza; “Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,”
No comments:
Post a Comment