Ufaulu kwa watahiniwa wa mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84
mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo
ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde
ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo,
msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya
Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao 10,
watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani Shinyanga, wawili
Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera.
Dk Msonde alisema jumla ya
watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata
jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250.
“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu
ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana
271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwapo ongezeko la ufaulu
kwa asilimia 2.52,”alisema Dk Msonde.
Watahiniwa 16,929 wamepata daraja
A, watahiniwa 141,616 wamepata Daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C,
watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E .
Dk Msonde alisema ufaulu katika
masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06 na
14.76 ikilinganishwa na mwaka 2015 huku masomo ya Kiswahili, Hisabati na
Kiingereza ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 0.39 na 12.51 ukilinganisha na
mwaka jana.
“Watahiniwa wamefaulu zaidi katika
somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 76.81 na somo walilofaulu kwa
kiwango cha chini ni Kiingereza lenye ufaulu wa asilimia 36.05,” alifafanua Dk
Msonde.
Dk Msonde aliwataja watahiniwa
waliofanya vizuri na shule zao kwenye mabano kuwa ni:
·
Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema),
·
Justina na Shabani Mavunde (Tusiime),
·
Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto
(Kwema)
·
Azad Ayatullah (Kaizirege).
Wasichana 10 bora:
1.
Justina Gerald (Tusiime)
2.
Danielle Onditi (Tusiime)
3.
Linda Mtapima (Kaizirege),
4.
Cecilia Kenene (Mugini),
5.
Magdalena Deogratias (Rocken Hill),
6.
Asnath Lemanya (Tusiime),
7.
Fatuma Singili (Rocken Hill),
8.
Ashura Makoba (Kaizirege),
9.
Rachel Ntitu (Fountain of Joy),
10.
Irene Mwijage (Atlas)
Wanafunzi wavulana 10 bora kitaifa,
1.
Japhet Stephano (Kwema),
2.
Jamal Athuman (Kwema),
3.
Enock Bundala (Kwema),
4.
Shabani Mavunde (Tusiime),
5.
Jacob Wagine (Kwema),
6.
Isaac Isaac (Kwema),
7.
Daniel Kitundu (Kwema),
8.
Benjamin Benevenuto (Kwema),
9.
Azad Ayatullah (Kaizirege)
10.
Benezeth Hango (Kwema).
Shule 10 bora ni:-
1.
Kwema (Shinyanga),
2.
Rocken Hill (Shinyanga),
3.
Mugini (Mwanza),
4.
Fountain of Joy (Dar es Salaam),
5.
Tusiime (Dar es Salaam),
6.
Mudio Islamic (Kilimanjaro),
7.
Atlas (Dar),
8.
St Achileus (Kagera),
9.
Giftskillfull (Dar),
10.
Carmel (Morogoro).
Shule 10 ambazo hazikufanya vizuri
ni:-
1.
Mgata (Morogoro)
2.
Kitengu (Morogoro)
3.
Lumba Chini (Morogoro),
4.
Zege (Tanga),
5.
Kikole (Tanga),
6.
Magunga ya Morogoro,
7.
Nchinila (Manyara),
8.
Mwabalebi (Simiyu)
9.
Ilorienito (Arusha)
10.
Chohero (Morogoro)
Mikoa 10 iliyoongoza kitaifa ni
Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha,
Njombe na Tabora wakati Halmashauri 10 bora ni Mpanda Manispaa, Geita Mji,
Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji, Mji Makambako, Ilemela
na Hai.
No comments:
Post a Comment