Tiba Ya Miguu
Kuwaka Moto:
1. Chukua majani ya mti wa
Mvumbasi, unguza pamoja na majani ya mti wa
mnungunungu, halafu changanya na mafuta ya taa
lita moja. Matumizi: Utakuwa unatumia kujichua kwenye
miguu kutwa mara tatu kwa muda wa
siku thelathini. Utapata nafuu kubwa sana.
Tunda aina ya mtopetope
2. TIBA YA KIKOHOZI:
Tafuna majani ya mti wa mbaazi. Mbali na
kutibu kikohozi, mti wa mbaazi, unatibu magonjwa
mengine mengi. Mfano, mizizi ya mti wa mmbaazi,
husaidia kutibu chango la kiume na kusafisha
kibofu cha mkojo.
3. KUVIMBA KWA TEZI LA SHINGO: Kama una sumbuliwa na
tatizo la tezi kuvimba, chukua unga wa Kamun
Nyeusi, kisha changanya na sega la nyuki, halafu
tumia kukanda kwenye tezi, kila siku kwa muda wa
mwezi mmoja. Utapata mafanikio makubwa sana.
4. TIBA YA MAUMIVU YA MGONGO, MIGUU,
NYONGA NA KIFUA KUPASUA:
Kama una
sumbuliwa na maumivu ya mgongo, miguu, nyonga
na kifua kupasuka, fuata maelekezo yafuatayo:
Chukua
mafuta ya nyonyo robo lita, mafuta ya Kamun Nyeusi
kiasi cha robo lita pamoja na mafuta ya karafuu robo
lita , changanya pamoja halafu uwe unatumia
kujichua sehemu yenye maumivu, kutwa mara tatu kwa
siku thelathini. Utapata nafuu kubwa sana.
5. TIBA
YA KWIKWI : Kama unasumbuliwa na kwikwi, fuata
maelekezo yafuatayo : Chukua majani ya mwembe mkavu,
pekecha kisha mpe mgonjwa atumie kuvuta
kama sigara halafu awe anameza moshi. Tatizo
la kwikwi litaisha.
6. Tatizo
La Kukojoa Kitandani ; Kama una
tatizo la kukojoa kitandani, tumia mizizi ya
mbaazi kwa kuchemsha, na kunywa maji yake
kutwa mara mbili kwa siku, kwa muda wa siku kumi
na nne.
7. Tatizo
la uvimbe kwenye kizazi : Kama una
tatizo la uvimbe kwenye kizazi, chukua
mizizi ya mtopetope, tumia kwa kuchemsha na kisha
kunywa maji yake, mara tatu kutwa kwa siku
thelathini.
8. Vidonda
vya koo : Kama una tatizo la vidonda
vya koo, chukua maji ya uvuguvugu kiasi cha nusu
lita, kisha kamulia ndimu tatu fresh, halafu
tumia kusukutulia. Utafanya hivyo mpaka, utakapo
pata nafuu.
9. Malaria
sugu : Kama una malaria sugu, chukua maji
ya dafu moja, weka kwenye chombo kisafi, kisha
kamulia ndimu saba, halafu tumia kunywa. Fanya
hivyo mara mbili kwa siku, asubuhi na
jioni kwa siku tatu hadi saba. Hakika
utapata matokeo mazuri sana.
10. Tiba
ya tatizo la kutoa harufu mbaya kinywani, sehemu
za siri, kikwapa na jasho lenye harufu mbaya :
Chukua maji yaliyo lowekewa mchele
kiasi cha lita moja, kisha tumia kunawia
sehemu husika na kusukutulia mdomo. Utafanya
hivyo mara tatu kwa siku hadi utakapo
ridhika na matokeo unayo yahitaji.
11. Kwa
wakina mama; Jinsi yakuzuia uchungu wamimba,maumivu yakiuno,
maumivu wakati wahedhi, na damu itokayo bila mpangilio wasiku maalumu,Chukua
majani ya mbigili yatwange halafu changanya navijiko vitatu vikubwa
vya unga wa mti unaitwa msonobali kisha tumia kunywa glasi 1
yenye ujazo wa milimita mia mbili na
hamsini, kutwa mara tatu hadi hali yako
itakapokua nzuri
12. Tiba
Ya Vidonda Vya Tumbo,Kisukari pamoja na
Typhoid:
Chukua mizizi ya mti wa msongati
pamoja na majani ya mkalatusi vitwange kwa pamoja kisha
chemsha kwenye maji lita moja, halafu tumia
kunywa glasi moja ya robo lita, mara tatu kwa
siku kwa siku thelathini.
13. Tiba
Ya Tatizo La Kukosa Hamu Ya Tendo La
Ndoa Kwa Wanawake : Kama wewe
ni mwanamke unaye sumbuliwa na tatizo
la kukosa hamu ya tendo la ndoa,
unaweza kutibu tatizo lako kwa kutumia vyakula
mbalimbali kama ifuatavyo :
i. JUISI
YA MIWA : Tumia kunywa nusu lita
hadi lita moja ya juisi ya miwa, mara
tatu kwa siku asubuhi, mchana na jioni kwa
siku thelathini. Utapata matokeo mazuri. Mbali na
kuwasaidia akina mama wenye tatizo la kukosa
hamu ya tendo la ndoa, juisi ya miwa
ina faida nyingine nyingi kitabibu. Moja kati
ya faida kubwa za juisi ya miwa, ni
uwezo wake mkubwa wa kusafisha figo. Hivyo
hata wanaume wanashauriwa kutumia juisi ya
miwa au miwa kwa wingi,kwa sababu
inasaidia kusafisha figo, na figo ni moja
kati ya ogani muhimu sana katika
mfumo wa nguvu za kiume.
ii. MBEGU
ZA FENESI : Chukua mbegu za fenesi kiasi
cha robo kilo, kisha chemsha na maji lita
mbili, halafu tumia kula pamoja na supu yake.
Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa
muda wa siku thelathini. Hakika utapata
matokeo mazuri sana. Unaweza pia kuzisaga
na kutumia unga wake, kwa kuchemsha na kunywa,
kwa kufuata utaratibu huo hapo juu.
iii. KOROSHO :
Tumia kula korosho pakti moja yenye ujazo
wa robo kilo, mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana
na jioni kwa siku thelathini. Yaani asubuhi,
tumia robo kilo, mchana robo kilo na jioni
robo kilo kwa siku thelathini. Utapata matokeo mazuri.
iv. MIHOGO
MIBICHI : Tumia kutafuna walau vipande
vitatu vya mihogo mibichi kwa siku, kwa
muda wa siku thelathini. Yaani asubuhi
utumie kipande kimoja kikubwa,mchana kipande
kimoja kikubwa na usiku, utumie kipande
kimoja kikubwa.
14. TIBA
ASILIA YA TATIZO KIFUA KISICHO PONA KWA WATOTO
WADOGO WALIO KUNYWA UCHAFU WAKATI WA KUZALIWA, PUMU, KIFUA KISICHO PONA
KWA WATU WAZIMA,KICHOMI,KUWASHWA MWILI NAKUPALIWA WAKATI UMELALA USINGIZINI
Tiba Yake, chukua
majani ya mpera kiasi cha kama viganja vinne,
yaponde pamoja na magome ya muembe kiasi cha
viganja vinne, na tunda la koma manga, twanga vyote
kwa pamoja ( Yani majani ya mpera, magome
ya muembe na tunda moja la komamanga ).
Ukisha maliza kutwanga,
changanya na maji lita mbili halafu chemsha
pamoja na lita moja ya asali mbichi ya
nyuki wadogo.
Chemsha hadi itokote,
halafu ipua dawa yako.
Matumizi :
Kwa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya
mwaka mmoja na miaka mitano, tumia kumpa kijiko
kimoja kikubwa mara mbili kwa siku, asubuhi
na jioni n kwa siku saba.
Na kwa mtu mzima, tumia kunywa vijiko
vikubwa viwili mara mbili kwa siku asubuhi
na jioni, kwa siku ishirini na moja
15. KUJITIBU
TATIZO LA MTOTO WA JICHO :
Kujitibu mtoto wa jicho, tumia kunyunyizia
jichoni matone mawili ya utomvu wa toto la ndizi.
Fanya hivyo mara tatu kwa siku, asubuhi,
mchana na jioni kwa siku thelathini. Utapata
matokeo mazuri.
Mbali na kutibu
tatizo la mtoto wa jicho, toto la ndizi, likichanganywa
kitaalamu na wine ya mnazi ( Palm wine ) au
mnazi, husaidia kutibu tatizo la kidole
tumbo au appendix.
16. TIBA
ASILIA YA KUPUNGUZA GESITUMBONI
Kuondoa gesi tumboni,
kwa kutumia tiba asilia, chukua juisi ya kitunguu maji kiasi
cha glasi moja yenye ujazo wa milimita mia
mbili na hamsini,kisha changanya na asali mbichi kijiko
kimoja koroga halafu tumia kunywa .
Utafanya hivyo mara tatu kwa
siku kwa muda wa siku kumi na nne.
AU chukua kipande
kimoja cha tangawizi,kiponde ponde kisha chemsha
kwenye nusu lita ya maji pamoja na kijiko kimoja
kikubwa cha asali mbichi ya nyuki wadogo,
halafu tumia kunywa kutwa mara mbili kwa
siku ishirini na moja.
AU ; Chukua asali
mbichi ya nyuki wadogo kiasi cha robo
lita, changanya na vijiko vitatu vikubwa
vya unga wa Kamun nyeusi,kisha chemsha pamoja
kwenye maji lita moja.Halafu tumia kula vijiko
vikubwa vitatu kutwa mara tatu kwa siku
ishirini na moja.
17. TIBA
YA PUMU : Chukua magadi vijiko vikubwa vitatu,
saga upate unga wake, kisha changanya na samli ya
n’gombe vijiko 21 vikubwa na asali vijiko 30
vikubwa. Matumizi : Tumia kula vijiko vikubwa
vitatu asubuhi, vitatu jioni na vitatu usiku kwa
muda wa siku thelathini. Utapata nafuu
kubwa sana.
18. TIBA
ASILIA YA KIHARUSI NA KIFAFA:
Chukua mizizi mitatu
ya mti wa ukwaju, mizizi mitatu ya
mti wa mkungu, mizizi mitatu ya mpapai, pamoja
na mizizi mitatu ya mti wa ufwambo.
Iponde ponde yote kisha chemsha kwa
pamoja kwenye maji ya lita tatu hadi
yachemke. Tumia kumpa mgonjwa glasi moja, kutwa
mara tatu kwa siku thelathini. Mgonjwa wako
atapata nafuu kubwa sana.
19. TIBA
ASILIA YA FANGASI ZA KWENYE DAMU, UKURUTU, UPELE, MCHAFUKO WA DAMU,
PAMOJA NA KUWASHWA KWAMWILI.
Chemsha robo kilo
ya majani ya mti wa mdimu kwenye maji kiasi
cha lita mbili. Maji yakisha tokota, ipua chuja,
halafu tumia kunywa glasi mbili asubuhi, mbili
mchana, mbili jioni. Utafanya hivyo kwa muda
wa siku thelathini. Hakika utapata nafuu
kubwa sana.
20. TIBA
ASILIA YA MARADHI YA FANGASI ZA MIGUU NA KUNUKA
MIGUU.
Twanga majani ya
mwarobaini robo kilo, chemsha na maji lita
tano, kisha weka kwenye beseni halafu loweka
miguu yako ndani ya beseni kwa muda wa
lisaa limoja. Utafanya hivyo kutwa mara mbili kwa
muda siku kumi na nne. Utapata matokeo
mazuri sana.
AU chukua majivu kiasi
cha robo kilo,changanya na robo lita ya juisi
ya ndimu, kisha nyunyizia kwenye miguu, na ukae
kwa lisaa limoja. Utafanya hivyo mara mbili kwa
siku kwa siku thelathini. Japo inauma lakini ni
tiba nzuri sana.
21. KUONGEZA MAZIWA
KWA MAMA ANAE NYONYESHA : Chukua
majani ya mti wa ukwaju, kiasi cha nusu
kilo, kisha chemsha na maji lita tano. Tumia
kunywa glasi tatu asubuhi, tatu mchana, tatu jioni kwa
muda wa siku saba. Hakika utapata matokeo
mazuri sana. Utakuwa unafanya hivyo kila
mara utakapo hitaji kuongeza maziwa.
MAKALA HAYA
YAMELETWA KWENU KWA HISANI YA NEEMA HERBALIST
& NUTRITIONAL FOODS CLINIC. DUKA LA KUUZA
DAWA MBALIMBALI ZA ASILI.
TUNAPATIKANA
UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM, JIRANI NA
SHULE YA MSINGI,UBUNGO NATIONA HOUSING NYUMA
YA JENGO LA UBUNGO PLAZA.
KWA MAHITAJI YAKO YA
DAWA MBALIMBALI ZA ASILI ZINAZO TIBU
MAGONJWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA,
WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0766 53 83 84.
NA KWA TAARIFA
ZAIDI KUHUSU HUDUMA ZETU, TEMBELEA KILA SIKU
KATIKA BLOGU YETU.
No comments:
Post a Comment