Tarehe Kama ya leo mwaka Jana,
ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania
kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.
Naamini nilileta sura na msisimko
mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu
Demokrasia maana yake ni nini.
Napogeuka nyuma kuingalia siku ile,
nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha
matumaini makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke
wangu Regina wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.
Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman
Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa
kasi mpaka visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.
Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya
uchaguzi, tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa
yaliyokwisha mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati
ule kwanini tunataka mabadiliko,hivi sasa kila mtu anakiona.
Pamoja na mafanikio machache katika
baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu
linalosubiri kulipuka,Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa
umma umekuwa kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana
kuwasweka ndani madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.
Nawashukuru sana wananchi kwa imani
kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla.Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo
wa uchaguzi mwengine, kwahiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza.Kasi,nguvu, ari
na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.
No comments:
Post a Comment