Wakali Kwanza, kundi lililowahi kutikisa mawimbi ya redio na TV nchini
kwa nyimbo kama Natamani na zingine, linatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia
kazi mpya iitwayo ‘Siishiwi Hamu.
Q-Jay
ambaye ni mmoja wa members watatu wa kundi hilo wakiwemo Makamua na Joslin,
alikiambia kipindi cha Mdundo Bado cha Lake FM kuwa kundi lao bado lipo pamoja
na imara.
Q amesema baada ya kuachia mradi wa
pamoja wa Wakali Kwanza ataachia pia kazi yake kama solo. Amedai kuwa Siishiwi
Hamu itatoka pamoja na video yake na ni wimbo uliofanyika MJ Records.
Ukimya wake Q Jay amedai kuwa
ulitokana na kuamua kumrudia mwenyezi Mungu lakini kutokana na kuupenda muziki
ameamua kuendelea na muziki wa kawaida lakini wenye mafundisho zaidi.
No comments:
Post a Comment