Serikali ya Gambia imesema kuwa
itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na
Waafrika pekee.
Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya
Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi
nchini humo mwaka 1994.
Uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka
huu viongozi nane wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa
kuhusika katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty
limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za
binadamu nchini Gambia.
No comments:
Post a Comment