Nilikuwa nategemea kuna siku kama hii itafika. Tangu Jay Z na Beyonce
watose kuhudhuria harusi ya Kanye West na Kim Kardashian miaka miwili
iliyopita, urafiki wa Yeezy na Hov uliingia matatani.
Wawili
hao kila mmoja amekuwa na maisha yake na kinachowaunganisha sasa ni mtandao wa
Tidal wanaoumiliki pamoja, lakini hakuna urafiki tena.
Na sasa Kanye yamemfika shingoni na
ameamua kuyatoa. Akiwa kwenye show ya ziara yake ya Saint Pablo huko Seattle,
Yeezy amemchana Hov kwa masuala kibao, kikazi hadi kifamilia.
Amelalamika kuwa watoto wao, hata
hawajahi kukutana na kucheza pamoja licha ya kile wanachokiamini kuwa ni
marafiki. “I can’t take this shit, bro,” alisema katikati ya show hiyo.
“Our kids ain’t never even played
together.”
Yeezy alimchana pia Jigga kuwa
asimpigie simu kumpa pole kwa mkasa wa mkewe kuvamiwa na kuporwa huko Paris,
bali anatakiwa kwenda nyumbani kwake na kumsalimia.
“You wanna know how I’m feeling?”
Don’t call me, after the robbery, and say ‘how you feelin?’ You wanna know how
I’m feelin? Come by the house. Bring the kids by the house like we brothers.
Let’s sit down.”
Pia Kanye alizungumzia uadui wa
Tidal na Apple unaomkera ambao anaamini unazuia mambo mengi, huku akimtupia
lawama Jay Z kuwa chanzo. Alieleza pia kuwa mashabiki wasitarajie album
nyingine ya Watch the Throne.
No comments:
Post a Comment